Waandamanaji na vyombo vya usalama wamekabiliana katika miji kadhaa ya Iran, watu 6 wakiripotiwa kupoteza maisha, ikiwa ni vifo vya kwanza tangu kuanza kwa maandamano ya raia kupinga kupanga kwa gharama za maisha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maandamano haya yalianza Jumapili iliyopita mjini Tehran ambako wauza maduka walifanya mgomo na kujitokeza barabarani kupinga bei za vitu kupanda na kudorora kwa uchumi, mgomo ambao sasa umeenea nchi nzima.
Hapo jana shirika la habari la Iran, Fars liliripoti vifo vya watu wawili kwenye mji wa Lordegan na Bakhtiari, huku wengine watatu wakiripotiwa kuuawa katika mji wa Azna baada ya makabiliano na polisi.

Mamlaka nchini humo zimethibitisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, huku zaidi ya 30 wakiripotiwa kutiwa nguvuni kutokana na kile polisi imesema walihusika kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.
Haya ni maandamano mengine makubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo, ambapo kwa yaliyopita, utawala uliyaita uhalifu, hata hivyo maandamano ya juma hili yakithibitisha hali ya kiuchumi inayokabili taifa hilo ambalo liko chini ya vikwazo vya Merekani na nchi za Ulaya.