Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeishtumu Rwanda kwa kuwauwa raia wa kawaida 1,500, Mashariki mwa DRC tangu mapema mwezi Desemba mwaka 2025.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Kinshasa, inasema tangu waasi wa M23/AFC wanaoungwa mkono na Rwanda, waanzishe vita vipya dhidi ya jeshi la FARDC, Mashariki mwa DRC, watu wengi wamepoteza maisha na wengine kuyakimbia makaazi yao.

DRC inasema watua hao waliuawa, baada ya kushambuliwa kwa mabomu na ndege zisizo na rubani aina ya kamikaze.

Vita hivyo, vilizuka muda mfupi baada ya viongozi wa DRC na Rwanda kutia saini mkataba wa kusitisha vita, jijini Washington, lakini waasi wa M23/AFC waliuteka mji wa Uvira, unaopakana na Burundi.

Mbali na mauaji, hayo, ripoti ya serikali ya Kinshasa, inasema maelfu ya watu wameyakimbia makaazi yao, wengi wakikimbilia Burundi, ambayo imefunga mpaka wake.

Rwanda imeendelea kukanusha madai ya serikali ya DRC, ikisisitiza kuwa haihusiki na utovu wa usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *