
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Afrika Kusini, unatarajiwa kuwa mgumu mwaka wa 2026. Sababu: Kurudi kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House na kuthibitishwa, mnamo Desemba 19 na Baraza la Seneti la Marekani, kwa uteuzi wa Leo Brent Bozell kama balozi mpya wa Marekani nchini Afrika Kusini. Uteuzi wenye utata, katika muktadha ambao tayari unakabiliwa na tofauti za kisiasa na kidiplomasia kati ya Washington na Pretoria.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Brent Bozell ambaye aliteuliwa na Donald Trump mwezi Machi, ni mtu maarufu wa mrengo wa kulia wa kihafidhina wa Marekani na mfuasi mkubwa wa Israel. Katika miaka ya 1980, alikuwa mwanachama wa kundi la shinikizo lililopinga mazungumzo yoyote na ANC, wakati huo kundi la harakati za ukombozi zilizoongozwa na Nelson Mandela na lilitangazwa wakati huo kama kundi la kigaidi na baadhi ya serikali za Magharibi.
Uthibitisho wake ulihitaji hatua kadhaa za kisheria, ikiwa ni pamoja na kusikilizwa mbele ya Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Seneti mnamo mwezi Oktoba, kabla ya kupigiwa kura ya mwisho siku ya Jumatano, Januari 31. Uteuzi huu unakuja huku nafasi ya balozi wa Afrika Kusini huko Washington ikiwa wazi tangu mwezi Machi, wakati Ebrahim Rasool aliporejeshwa Pretoria baada ya kuelezea sera ya Marekani kama “wazungu ni bora kuliko watu wa jamii zingine.”
Pigo kwa uhusiano kati ya Washington na Pretoria
Tangu mwezi Februari 2025, Donald Trump amekata msaada kwa Afrika Kusini, ambayo anaishutumu kwa kuwatendea vibaya wazungu wachache kwa sheria yake ya hivi karibuni ya unyang’anyi. Pia katika kesi nyingine ambayo Washington inaishtumu Pretoria ni malalamiko ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kwa mauaji ya kimbari huko Gaza mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Leo Brent Bozell ameonyesha kwamba anakusudia kushinikiza mamlaka ya Afrika Kusini kuondoa malalamiko hayo.
Utawala wa Marekani ulikataa kushiriki katika mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika Johannesburg mwezi Novemba na pia uliiondoa Afrika Kusini katika orodha ya nchi zilizoalikwa kwenye mkutano ujao wa G20, ambao utafanyika Marekani.
Huko Pretoria, kuwasili kwa Leo Brent Bozell, “mgeni katika uhusiano wa kimataifa” na “asiye na uzoefu na bara la Afrika,” kwa hivyo kunaonekana kwa mashaka, anabainisha mtafiti mmoja. Faida yake pekee inaonekana kuwa ni msimamo wake wa kiitikadi na rais wa Marekani.