Wasafiri na wasafirishaji wanaotumia barabara ya Mtwara–Newala–Masasi yenye urefu wa takribani kilomita 160, wameeleza kero zao kuhusu changamoto zinazojitokeza wakati wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Wananchi wanasema michepuo ya barabara inayowekwa na mkandarasi imekuwa kikwazo kikubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo, hususan katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.
Kwa mujibu wa wasafiri hao, michepuo hiyo husababisha magari kuchelewa, kuharibika, na wakati mwingine kushindwa kabisa kupita, hali inayowaathiri wananchi kufika katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi kwa wakati.
✍John Kasembe
Mhariri | @claud_jm
#azamtvupdates