Wiki za mwisho za mwaka 2025 ziliangaziwa na mvutano mpya kati ya Misri na Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa zamani wa kivita mashariki mwa Libya, ambaye anadhibiti eneo hilo na kusini mwa Libya. Katikati ya mzozo huo ni ushiriki wa Haftar katika mzozo wa Sudan.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Cairo, Haftar, akihimizwa na Abu Dhabi, anatoa msaada wa vifaa kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambavyo vinapigana dhidi ya jeshi la serikali. Kwa hivyo, Kusini mwa Libya imekuwa kituo usaidizi, kinachosafirisha silaha, mafuta, na mamluki kupitia Darfur. Misri, ikiwa na wasiwasi kuhusu mipaka yake ya kusini na magharibi, inazidisha juhudi zake za kidiplomasia kumshawishi Haftar kusitisha vitendo vyake.

Uhusiano kati ya Cairo na Haftar umekuwa mgumu tangu msimu wa joto wa mwaka 2023. Mnamo mwezi Juni, Cairo ilimwalika Saddam Haftar, naibu kamanda wa baadaye wa Jeshi la Kitaifa la Libya, akitumaini “kusitisha hali hiyo.” Licha ya mapokezi ya kifahari, mkutano huo ulishindwa kutatua mzozo uliokuwapo.

Kinyume chake, mamlaka mashariki mwa Libya iliongeza usaidizi wao kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Misri inajikuta ikishindana na mataifa mengine yenye nguvu za kikanda, yote yakitaka kumvuta Haftar katika nyanja yao ya ushawishi.

Mnamo Desemba 8, Khalifa Haftar na wanawe wawili, wote wakiwa maafisa wa kijeshi, waliitwa Cairo. Kulingana na vyombo vya habari vya Misri, Rais al-Sisi aliwakemea. Msemaji wa rais alisema kwamba “usalama wa Sudan una uhusiano wa karibu na ule wa Misri na Libya” na akalaani uingiliaji wowote wa kigeni pamoja na uwepo wa mamluki.

Licha ya maonyo haya, Haftar bado ni anasita kubadilika. Siku ya Jumatatu, Misri ilimtuma naibu mkuu wake wa ujasusi kwenda Tripoli pamoja na ujumbe wa usalama, ambao ulikutana na Waziri Mkuu Dbeibah. Mpango huu una malengo mawili: kumkumbusha Haftar kuhusu mipaka ya vitendo vyake huku ukionyesha kwamba Misri ina njia mbadala nchini Libya.

Sasa kwa kuwa mzozo umeanzishwa, na Saudi Arabia na UAE zinapingana hadharani nchini Yemen, Misri inaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuingilia kati, kwa kuongeza shinikizo kwa mshirika wake mashariki mwa Libya, ambaye hataki kubadilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *