
Kiongozi wa Venezuela Nicolas Maduro aliyetekwa kwa nguvu na vikosi vya jeshi la Marekani wiki iliyopita, amefikishwa Mahakamani jijini New York pamoja na mkewe Cilia Flores, ambako wamefunguliwa mashtaka ya kuwezesha biashara ya dawa za kulevya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maduro mwenye umri wa miaka 63, na mkewe, wote wamekanusha mashtaka yanayowakabili nchini Marekani.
Akiwa amevalia mavazi ya mfungwa, Maduro amesema hana kosa na kusisitiza kuwa yeyé bado no rais wa Venezuela.
Aidha, ameiambia Mahakama kuwa, amejikuta nchini Marekani, baada ya kutekewa Januari tarehe tatu, akiwa nyumbani kwake jijini Caracasa.
Baada ya kufikishwa Mahakamani kwa mara ya Kwanza, na kukanusha shutuma dhidi tao, Maduro na mkewe wanatarajiwa kurejeshwa Mahakamani Machi tarehe 17.
Wakati akifikishwa Mahakamani, jijini Caracas maelfu ya wafuasi wake waliandamana kumuunga mkono, huku naibu wake Delcy Rodriguez, akiapishwa kuwa rais wa mpito.
Rais Donald Trump amesema, nchi yake itaisimamia Venezuela na kumwonya kiongozi wa mpito kuwa, atalipia gharama kubwa iwapo atakwenda kinyume na matarajio ya Marekani.
Katika hatua nyingine, hatua ya kutekwa kwa Maduro, kumewagawa wabune na Maseneta nchini Marekani, ambako chama cha upinzani cha Democratic, kimeshtumu namna opersheni hiyo ilivyofanyika.