#HABARI: Timu ya Taifa ya Kandanda ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo ilikuwa irejee nchini kesho Januari 07, 2025 sasa itarejea Januari 08, 2026.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesema mabadiliko hayo yana lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwasili muda mzuri ambao utatoa nafasi kwa Watanzania kuwapokea na kuwapongeza wachezaji kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya wakiwa katika mashindano makubwa ya kandanda Barani Afrika (AFCON2025) yanayofanyika nchini Morocco.
Kulingana na mabadiliko hayo sasa Taifa Stars itawasili nchini keshokutwa majira ya saa 4:00 asubuhi na kupokelewa na wananchi wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi.
Msigwa ametoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kujitokeza kuwashangilia na kuwapongeza mashujaa hao Taifa Stars kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya nchini Morocco.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.