#HABARI: Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umezindua mkakati wa kupita “Banda kwa Banda” ili kuwafikia na kuwahudumia wanachama wake katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Afisa Uhusiano wa PSSSF, Bi. Regina Kumba, ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuwasaidia watumishi wa umma wanaotoa huduma kwenye mabanda mengine ambao hawapati nafasi ya kwenda kwenye banda la PSSSF kupata elimu na huduma.

Bi. Kumba amefafanua kuwa kwa sasa huduma nyingi za mfuko huo zinapatikana kidijitali kupitia PSSSF Portal, ambapo mwanachama anaweza kujihudumia mwenyewe kwa kutumia simu janja au kompyuta.

Kupitia ziara hiyo ya banda kwa banda, maafisa wa mfuko huo wanatumia fursa hiyo kuwapa watumishi elimu ya vitendo ya jinsi ya kujiunga na kutumia mfumo huo rahisi uliopo viganjani mwao.

Nao wanachama waliofikiwa na huduma hiyo, akiwemo Bw. Mulegi Majogoro kutoka Wizara ya Habari na Bw. Natalis Liduma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, wameupongeza mfuko huo na serikali kwa kuboresha mifumo ya kidijitali.

Wamesema huduma hiyo imewarahisishia kupata taarifa zao kwa haraka na kutatua changamoto zao bila kulazimika kuondoka kwenye maeneo yao ya kazi maoneshoni.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *