#HABARI: Familia zilizoathirika na mafuriko yaliyosababisha zaidi ya Kaya 400 kukosa makazi, wilayani Kilosa mkoani Morogoro, zimekabidhiwa msaada wa tani tano za sukari ya Bwana Sukari na Kampuni ya Kilombero Sugar iliyoko mkoani humo.
Msaada huo umetolewa kupitia Mpango wa Msaada wa Dharura wa kampuni hiyo na umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka, kwa niaba ya waathirika wa mafuriko hayo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, wawakilishi wa Kilombero Sugar wamesema kampuni inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kijamii kwa kushirikiana na mamlaka za Serikali na jamii katika nyakati za changamoto.
Uongozi wa Wilaya ya Kilosa umeshukuru msaada huo, ukisema utasaidia familia zilizoathirika kurejea katika hali ya kawaida huku juhudi za Serikali za kuwasaidia zikiendelea.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.