Waangalizi wa kimataifa, wakiwemo Umoja wa Afrika na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSCA), walisema siku ya kupiga kura kulikuwa na amani kwa kiasi kikubwa, licha ya kuwepo kwa changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa nchi.
Hata hivyo, muungano mkuu wa vyama vya upinzani unaojulikana kama Republican Bloc for the Defence of the Constitution ulisusia uchaguzi huo, ukidai kuwa haukuwa wa haki.
Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi huo, wakiwemo mawaziri wakuu wa zamani Anicet-Georges Dologuele na Henri-Marie Dondra, waliishutumu serikali kwa kuweka vikwazo katika kampeni, ikiwemo kuzuia safari za wagombea kwenda maeneo ya mikoani.
Mahakama ya Katiba ina hadi tarehe 20 Januari kuthibitisha rasmi matokeo hayo au kutoa uamuzi kuhusu pingamizi lolote litakalowasilishwa.