#HABARI: Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Kamani, ametoa agizo kwa Maafisa Mifugo na Uvuvi nchini kuhakikisha wanawafuata wafugaji na wavuvi katika maeneo yao ili kuwapatia huduma, badala ya kuwasubiri maofisini.
Akizungumza katika mkutano wa wafugaji, wavuvi na wadau wa sekta hizo uliofanyika wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu, Mhe. Kamani amesema Serikali inataka watumishi wote wa sekta hizo kufanya kazi kwa ukaribu na wananchi wanaowahudumia.
Amesisitiza kuwa Maafisa hao wanapaswa kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa wadau wao moja kwa moja mashinani, badala ya kuwasubiri ofisini kama ilivyokuwa desturi miaka iliyopita.
Kabla ya mkutano huo, Mhe. Kamani alitembelea shamba la mfugaji na mkulima wa malisho ya mifugo, Dkt. Mathias Abuya, na kuwataka wafugaji wengine kulitumia shamba hilo kama shamba darasa la kujifunzia mbinu bora za ufugaji na uzalishaji wa malisho.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.