Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), imeanza ukaguzi maalumu kwa waandishi wa Habari wasio na sifa wanaendelea na kazi kwa kuwa ni kosa kisheria.
Kwa mujibu wa Bodi hiyo, msako huyo utahusisha vyombo vya habari na maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujiridhisha kuwa watu wote wanaotekeleza majukumu ya kihabari wanakidhi vigezo vilivyoainishwa kwa mujibu wa sheria.
Taarifa ya Bodi hiyo inasema kiwa imebaini kuwa kuna baadhi ya watu wasio na sifa wamerejea kutekeleza majukumu ya kihabari baada ya uchaguzi mkuu.
“Bodi inatoa onyo na kuwataka watu wote wanaofanya kazi za kihabari bila kuwa na ithibati kuacha mara moja, kwani kuendelea kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 50(2)(b) cha sheria ya huduma za habari, sura ya 229,” imesema.