
Rasmussen aliyasema hayo alipokuwa katika ziara fupi mjini Kiev.
“Ukiniuliza mimi, (vikwazo) vinapaswa kuwa vigumu iwezekanavyo. Ni lazima iwe orodha ya vikwazo vinavyogusa pande zote, meli za mafuta ya Urusi na sekta ya fedha.”
Denmark inayoshikilia urais wa kupokezana wa miezi sita wa Umoja wa Ulaya itashinikiza kutolewa awamu ya 19 ya vikwazo kwa Urusi kabla ya muhula wake kumalizika mwezi Desemba.
Akizungumza pamoja na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Ukraine Andrii Sybiha, Rassmussen amesema anakaribisha mchango harakati zozote kutoka Marekani kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi.