
Nchini Venezuela, shambulio ambalo Marekani ilimteka nyara Nicolás Maduro na mkewe Cilia Flores lilisababisha vifo vya watu 100, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela Diosdado Cabello ametangaza siku ya Jumatano, Januari 7. Pia amesema kwamba rais wa Venezuela aliyeondolewa madarakani na mkewe walijeruhiwa wakati wa operesheni hiyo.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waziri Mkuu wa Venezuela Diosdado Cabello alitangaza kwamba watu wasiopungua 100 walifariki wakati wa shambulio kubwa lililopewa jina la “Absolute Resolve,” lililofanyika ndani ya saa tano tu usiku wa Januari 2 kamkia Januari 3, ambalo lilisababisha kutekwa nyara kwa rais Nicolas Maduro na mkewe, Cilia Flores.
Shambulio ambalo Marekani ilimteka nyara Nicolás Maduro huko Caracas lilisababisha vifo vya watu 100, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela Diosdado Cabello alitangaza Jumatano, Januari 7. “Hadi sasa, namaanisha hadi sasa, kuna watu 100 waliofariki, 100, na idadi kama hiyo imejeruhiwa. Shambulio dhidi ya nchi yetu lilikuwa baya sana,” Bw. Cabello alisema wakati wa kipindi chake cha kila wiki kwenye televisheni ya umma.
Vikosi vya jeshi vya Venezuela vilirusha video nyingi siku ya Jumatano kuhusu mazishi ya wanajeshi waliouawa wakati wa operesheni ya Marekani iliyosababisha kukamatwa kwa rais Nicolas Maduro. Katika video hizo wanaonekana ndugu kadhaa wakilia, majeneza yaliyofunikwa na bendera za Venezuela, hotuba za kusifu “ujasiri, ushujaa, heshima, na uaminifu” wa wanajeshi waliouawa… Shada za maua na taji za maua, pamoja na picha za marehemu, zilipamba majeneza, ambayo yalisindikizwa na wanajeshi wakiwa mafunzoni.
Nicolas Maduro na mkewe walijeruhiwa wakati wa kukamatwa kwao na jeshi la Marekani, kulingana na Caracas
Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores wote walijeruhiwa wakati wa kutekwa nyara na jeshi la Marekani, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela Diosdado Cabello alibainisha. “Cilia alijeruhiwa kichwani na kupata pigo mwilini. ‘Ndugu’ Nicolas alijeruhiwa mguuni. Kwa bahati nzuri, wanaedelea vizuri,” Cabello alisema wakati wa kipindi chake cha kila wiki kwenye televisheni ya umma.
Siku ya Jumatatu, Januari 5, wakati wa kufikishwa kwao kwa mara ya kwanza mbele ya jaji wa shirikisho la Marekani, wakili wa Cilia Flores, Mark Donnelly, alisema kwamba mteja wake alipata majeraha makubwa wakati wa shambulio hilo, akitaja michubuko mikubwa kwenye mbavu zake. Aliomba afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu na X-ray.