Waraka wa rais uliotiwa saini na Trump unaelekeza wizara na taasisi za serikali kusitisha ushiriki na ufadhili kwa mashirika 31 ya Umoja wa Mataifa “haraka iwezekanavyo.”

Kwa mujibu wa Ikulu ya White House mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na maslahi ya kitaifa ya Marekani, usalama wake, ustawi wa kiuchumi au uhuru wa kujitawala.

Hata hivyo amri hiyo haikubainisha ni kiasi gani cha fedha ambacho serikali ya Marekani inatarajia kuokoa kupitia kujiondoa huko.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema kwenye mtandao wa X kwamba Washington inajiondoa kwenye mashirika aliyoyataja kuwa yanayopinga Marekani, yasiyo na maana au yanayopoteza fedha na kwamba mapitio ya mashirika mengine ya kimataifa yanaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *