
Mageuzi ya nambari mpya za usajili wa magari kwa mfumo ulio salama nchini DRC, uliyotangazwa na Kurugenzi Kuu ya Ushuru, na ambayo yalianza kutumika rasmi Januari 6, 2026, yamesababisha kutoelewana na hasira miongoni mwa madereva na mashirika ya kiraia.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa
Wengi wanaogopa mzigo wa ziada wa kifedha, kufuatia kuanzishwa hivi karibuni kwa leseni za udereva za kibayometriki na ukaguzi wa lazima wa magari. Kutokana na utata huo, Wizara ya Fedha imefafanua maelezo ya operesheni hii, ikiwasilishwa kama ya taratibu na inayozingatia viwango vya kimataifa. Hii haijazingatia mwitikio wa mashirika ya kiraia, ambayo yanalaani mchakato usio wazi na usio na umuhimu mkubwa kwa Serikali.
Serikali inahalalisha mabadiliko haya kwa nia yake ya kupambana na kuenea kwa nambari za usajili wa magari bandia. Lakini tangazo hilo lilipingwa haraka na kukosolewa. Madereva wengi wameogopa kubadilishwa mara moja na kwa lazima kwa nambari zao za sasa za usajili wa magari, ingawa kuzipata bado ni vigumu katika mikoa kadhaa.
Kutokana na utata huo, Wizara ya Fedha imefafanua kwamba nambari mpya za usajili wa magari, kwa sasa, zitatumika tu kwa magari mapya. Yale ambayo tayari yanatumika yataendelea kuwa na nambari zao za sasa hadi mwisho wa 2026, wakati nambari mpya zitakuwa za lazima kwa magari yote.
Kutoka upande wa mashirika ya kiraia, muungano wa “Kongo Haiuzwi” (CNPAV) umelaani mchakato wa utoaji wa soko hili kama usio wazi. muungano huo unasema kna mashaka ya upendeleo, mpango wa kifedha usiofaa kwa serikali, na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa operesheni hiyo, pamoja na ukaguzi huru wa soko la nambari za usajili wa magari.
Soko hili lina faida kubwa. Kulingana na jukwaa la kupambana na ufisadi, nambari ya usajili wa gari, iliyotengenezwa nchini Ubelgiji kwa dola 35, itauzwa tena kwa serikali ya Kongo kwa dola 65. Madereva wataweza kuipata kwa dola 100, au hata dola 115.