Dar es Salaam. Miss Grands Tanzania 2025, Beatrice Alex ambaye pia ni balozi wa mchezo wa kubashiri wa Bang Bet ameweka wazi namna ambavyo kwa sasa jamii inamchukulia.
Akizungumza leo Januari 8,2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapatia zawadi ya pesa taslim na TV washindi wa ‘Bang Bet’. Beatrice amesema watu wanaomzunguka wanadhani tayari amekuwa tajiri na humshangaa akiwa na shida.
“Eeeeh watu wanafikiria mimi ni tajiri, namuomba Mungu nipate pesa ambazo watu wanafikiri ninazo. Watu wanakutegemea usiwe na shida, usiwe unapitia changamoto yaani wanategemea uwe kama malaika.
“Yaani kunakiwango cha maisha watu wanataka uishi unaona kabisa hiki kiwango ni cha watu matajiri mimi ni msichana tu mdogo nina jitahidi kufanya vitu vyangu kuna baadhi ya mawasiliano kwa baadhi ya watu unaelewa kabisa watu wanamaanisha nini,” amesema
Hata hivyo ameoesha utofauti wake na baadhi ya watu waliowahi kupita kwenye mashindano ya urembo kwani Beatrice anasema hajioni kabisa katika kufanya uigizaji wala muziki. Huku akiweka wazi baadhi ya vijana wanaogopa kumfuata kimahusiano licha ya kuwa taji lake halimruhusu kuolewa wala kupata ujauzito
“ Nafikiri hicho ni kikubwa kwa sababu kuna makubaliano ambayo mnaweka kuwa utakuwa unajitoa kwa jamii kwa asilimia na muda wote. Kwa sasa niko very Single ni kwa muda mrefu sijui ni kwa sababu gani watu hawanitongozi.
“Nina miezi michache ya kumaliza kwahiyo watu waje. Hapana sio kama niko kwenye kifungo umeona kama sasa hivi tupo busy na kazi naweza kusema ni mwaka wa kukimbizana,”amesema
Ikumbukwe yote hayo ni katika utolewaji wa zawadi hizo za Bang Bet ambao Ndebile Paulo mshiriki wa Bang Bet kutoka Singida ameibuka ameondoka na kitita Sh 5milioni na TV aina ya Hisense inch 55, huku Bakari Said na Manon William nao wakiibuka washindi wa TV hizo.
Mbali na Beatrice wengine waliokabidhi zawadi ni Meneja Biashara kutoka Mix by Yas Fabian Falician, akiwa na Meneja Masoko wa Bangbet, Lusekelo Mwandenene.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwandenene amesema kuwa promosheni ya Nogesha na Bangbet imelenga kuwapa fursa ya kuanza mwaka kwa kishindo washiriki.
“Leo ni siku maalumu kabisa ya kukabidhi washindi wetu zawadi. Katika kipindi cha mwezi wa 12 tulikuwa na kampeni yetu matata kabisa ya Nogesha na Bang Bet. Leo tumekabidhi mshindi wetu Sh 5milioni, pamoja na TV zaidi ya nane ambao leo waliokuja ofisini kwa ajili ya kuchukua zawadi zao ni washindi kadhaa kuna washindi wengine zaidi ya nane ambao wapo mikoani watapokea. Nogesha na Bang Bet inaendelea hadi mwezi wa tano,”amesema