Venezuela imeanza kuwaachia huru idadi kubwa ya wafungwa wa kisiasa, wakiweomo wageni kadhaa, katika hatua ya makubaliano na Marekani baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa nchi hiyo Nicholas Maduro.

Kuachiliwa huko kwa wafungwa kulikoanza jana Alhamisi ni kwa mara ya kwanza tangu makamu wa zamani wa Maduro, Delcy Rodriguez, alipochukua nafasi hiyo, kwa kuungwa mkono na rais Donald Trump wa Marekani, ambaye anasema ameridhika kumruhusu atawale ili mradi tu ataipa Marekani ufikiaji wa mafuta. 

Mgombea wa zamani wa upinzani wa Venezuela, Enrique Marquez — ambaye alimpinga Nicolas Maduro katika uchaguzi wa rais wa 2024 uliozozaniwa — alikuwa miongoni mwa walioachiliwa Alhamisi.

Hapo jana Trump alisema kiongozi wa upinzani wa Venezuela Maria Corina Machado atazuru Washington wiki ijayo, akiashiria anapanga kukutana na mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *