Kazuyoshi Miura anayetimiza miaka 59 mwezi Februari mwaka huu na kuwa mchezaji mkongwe zaidi wa soka duniani anajiunga na klabu mpya anapojiandaa kwa msimu wake wa 41. Nchini Japan kama “King Kazu.”

Miura alitangaza kusaini mkataba mpya wiki hii na timu ya Ligi daraja la tatu -J League – ya Fukushima United. Anahamia kwa mkopo akitokea Yokohama FC na msimu uliopita alicheza kwa mkopo na timu ya Atletico Suzuka, iliyoko daraja la nne.

Miura amekuwa mchezaji wa kulipwa nchini Brazil, Italia, Croatia, Australia na Ureno na  nchini Japan. Alianza kucheza kwa mara ya kwanza mwaka wa 1986 akiwa na klabu ya Santos nchini Brazil, ambayo mchezaji nyota taifa hilo, Edson Arantes do Nascimento “Pelé” aliipatia umaarufu mkubwa.

Kazuyoshi Miura (kushoto)
Kazuyoshi Miura alikuwa katika kikosi cha kwanza katika pambano la Yokohama FC dhidi ya Kawasaki Frontale akiwa na umri wa miaka 53Picha: JIJI PRESS/AFP/Getty Images

Mwaka 2017 alivunja rekodi akiwa na miaka 50

Mnamo 2017 akiwa na umri wa miaka 50, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mzee zaidi kufunga bao katika mechi inayofuatiliwa na shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA. Rekodi hiyo iliipiku ile ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Stanley Matthews aliyekuwa akisifiwa sana.

Miura lilikuwa moja ya majina makubwa na ya kwanza katika soka la Japan. Alifunga mabao 55 katika mechi 89 na alikuwa nyota katika timu ya taifa ya Japan miaka ya 1990.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *