
Jeshi la Sudan siku ya Ijumaa lilisema kuwa limewakabili vikali vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) wakati wa operesheni ya angani na ardhini katika kipindi cha wiki moja iliopita kwenye kanda za Darfur na Kordofan.
Katika taarifa, jeshi lilisema vikosi vyake vilifanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya RSF, kuharibu magari 240 ya kivita na kuwaua mamia ya wapiganaji.
Jeshi limesema operesheni hiyo pia ililenga kile walichokiita maeneo ya RSF ya mikakati, ikiwemo sehemu wanazorushia ndege zisizo na rubani na ya kuhifadhi silaha, pamoja na maeneo katika Uwanja wa Ndege wa Nyala Kusini mwa Darfur.
Iliongeza kuwa wamefanikiwa kuwatimua wapiganaji wa RSF kutoka katika maeneo yote ya Darfur na Kordofan, na kwamba operesheni ilikuwa bado inaendelea kuwasaka wapiganaji waliobakia.