Serikali imeweka ukomo wa miezi mitatu kwa taasisi zote ambazo bado hazijasajiliwa katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi(PDPC)kutii sheria, vinginevyo hatua za kisheria zitaanza kuchukuliwa.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, @angellah_kairuki , wakati akifunga mafunzo ya Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutoka taasisi za umma na binafsi jijini Arusha.

Waziri Kairuki amesema mafunzo hayo ni nyenzo muhimu ya kupunguza uhalifu wa taarifa binafsi, akisisitiza kuwa usalama wa faragha za wananchi ni sehemu ya usalama wa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *