Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulikatizwa mwaka wa 2019. Katika taarifa mbalimbali siku ya Ijumaa, Januari 9, viongozi wa Venezuela na Marekani walikiri nia yao ya kutafuta mwafaka wa kidiplomasia, ambao ulianzishwa na ziara ya ujumbe wa wanadiplomasia wa Marekani huko Caracas.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa, Januari 9, rais wa Marekani alikaribia kuanzisha shambulio jipya dhidi ya Venezuela. Shambulio hili lilifutwa, kulingana na Donald Trump, kutokana na “ushirikiano” wa Caracas na mamlaka ya Marekani. “Marekani na Venezuela zinafanya kazi vizuri pamoja,” alitangaza, hasa katika “ujenzi mpya” wa tasnia ya mafuta, rais alibainisha, saa chache kabla ya kukutana na wakuu wa sekta ya mafuta wa Marekani.

Baadaye siku hiyo, afisa wa Marekani aliarifu shirikala habari la AFP kwamba wanadiplomasia wa Marekani walisafiri hadi Caracas kufikiria kufungua tena ubalozi wa Marekani nchini Venezuela, ambao umefungwa tangu mwaka 2019. Wakati huo, Donald Trump, wakati wa muhula wake wa kwanza, alimtambua Juan Gaido kama rais wa Venezuela. Nicolas Maduro, akishutumu uingiliaji kati wa jirani yake wa kaskazini, kisha akakata uhusiano na kuwapa wanadiplomasia wa Marekani saa 72 kuondoka nchini, anaripoti mwandishi wetu huko Caracas, Alice Campaignolle.

John McNamara, mwanadiplomasia mkuu katika ubalozi wa Marekani katika nchi jirani ya Colombia, na wanadiplomasia wengine “walisafiri hadi Caracas kufanya tathmini ya awali kwa lengo la kuanza tena taratibu kwa” shughuli za kidiplomasia za Marekani nchini Venezuela, afisa huyo wa Marekani alisema.

Delcy Rodriguez anapendelea “njia ya kidiplomasia”

Taarifa hii ilithibitishwa na Venezuela. Katika taarifa, serikali ya Kaimu rais wa Venezuela Delcy Rodriguez ilitangaza kwamba “imeamua kuanzisha mchakato wa kidiplomasia wa uchunguzi na serikali ya Marekani, unaolenga kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.”

Katika mkutano wa mtandaoni na marais wa Brazil na Colombia, Luiz Inácio Lula da Silva na Gustavo Petro mtawalia, pamoja na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez, Kaimu rais wa Venezuela Delcy Rodriguez walilaani “uchokozi mkubwa, wa uhalifu, usiojikita kwenye sheria, na usio halali uliofanywa dhidi ya Jamhuri ya Venezuela.”

Pia alibainisha kwamba, ingawa nchi yake “si haiongozwi wala kuwa chini mamlaka” ya Washington, “Venezuela itaendelea kukabiliana na uchokozi huu kupitia njia za kidiplomasia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *