Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana siku ya Jumatatu kwa mkutano wa dharura wa kuijadili Ukraine. Hatua hiyo inakuja baada ya meya wa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Vitaliy Klitschko kuwasihi wakazi katika mji huo kuondoka mara moja kutokana na kukatika kwa umeme katika sehemu kubwa ya mji kufuatia mashambulizi ya droni na maroketi yanayofanywa na Urusi.

Meya huyo ameongeza kwamba mashambulizi ya Urusi ya hivi karibuni yaliacha nusu ya majengo ya makazi huko Kyiv bila nishati ya umeme hali inayoharatisha maisha yao hasa katika wakati huu wa msimu wa baridi kali ambapo halijoto iko chini ya sifuri.

Kwa upande mwingine mwakilishi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa, Andriy Melnyk amesema katika barua yake kwa Baraza la Usalama kwamba serikali yaUrusi imefikia kiwango kipya cha kutisha cha uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu nchini Ukraine.

Aidha, licha ya jitihada mbalimbali za kuvimaliza vita kati ya Urusi na Ukraine vya miaka minne sasa bado nchi hizo mbili zimeendelea kushambiliana kwa makombora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *