
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, wameapa kulinda mali ya umaa, wakati huu maandamano makubwa yakiendelea kwa siku kadhaa sasa dhidi ya serikali.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Onyo hili limekuja, wakati wakuu hao wa usalama wakisema watalinda miundo mbinu mbinu muhimu ya serikali na kuwataka raia wa Iran kuepuka kuingia kwenye mtego wa maadui wa nchi hiyo.
Aidha, hii inakuja baada ya rais Donald Trump, siku ya Ijumaa aliwaonya tena viongozi wa Iran, kuacha kuwelenga raia wanaoandamana, akisema Marekani ipo nyuma ya waandamanaji waliowaita mashujaa.
Kwa wiki ya pili sasa ambapo maandamano makubwa yamekuwa yakiendelea katika miji mbalimbali nchini humo, na kusababisha serikali kukata mtandao wa Internet na kuzuia mawasiliano kupitia laini za simu.
Watete wa haki za binadamu wanasema watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha na wengine wamejruhiwa, huku rais Trump akitishia kuishambulia Iran, iwapo vikosi vya usalama, vitanedelea kuwalenga raia.
Maandamano hayo yalianzia jijini Tehran kwa raia wa nchi hiyo kulalamikia kuapnda kwa gharama ya maisha, lakini yamegeuka na kuwa dhidi ya serikali inayoongozwa na rais Masoud Pezeshkian, aliyechaguliwa mwaka 2024.