
Michuano ya kandanda ya mataifa barani Afrika AFCON 2025 inayofanyika nchini Morocco inaendelea hii leo Jumamosi kwa hatua ya robo fainali katika mechi za siku ya pili ya hatua hiyo.
Mua mfupi ujao, mchezo wa awali utaanza kati ya Nigeria Super Eagles dhidi ya Algeria majira ya saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja Stade de Marekhesh.
Mabingwa wa mara nyingi wa michuano ya AFCON Mafarao wa Misri watashuka dimbani kumenyana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Ivory Coast katika uwanja wa Stade Adrar mjini Agadir.
Tayari wenyeji Morocco na Senegal zimetinga hapo jana na sasa zinasubiri mechi za leo kujua washindani wao katika mechi za hatua ya nusu fainali hapo Januari 14.