#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Agnes Amos Liku, mwenye umri wa miaka 35, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuhusiana na madai ya kujifungua mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha Mwanzomgumu, Kata ya Msimbu, Wilaya ya Kisarawe, mkoani humo.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salim Morcase, amebainisha kuwa kufuatia madai hayo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na madaktari bingwa lilichunguza tukio hilo na kubaini kuwa halikuwa na ukweli wowote juu ya kile alichokuwa akidai mtuhumiwa huyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na madaktari bingwa wawili wa magonjwa ya akina mama kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ulibaini kuwa Agnes hakuwa mjamzito wala hakuwa na dalili zozote za kujifungua.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa taarifa za uongo, na kusisitiza kuwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria, huku likibainisha kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.