
Upigaji kura uliongezeka hadi miji mingine ikiwemo baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya kijeshi na wapinzani wake wenye silaha.
Wakosoaji wanasema uchaguzi huo ulioandaliwa na serikali ya kijeshi si huru wala wa haki na ni juhudi za jeshi kuhalalisha utawala wake baada ya kunyakua madaraka kutoka kwa serikali iliyochaguliwa ya Aung San Suu Kyi mnamo Februari 2021.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo huru vya habari vya mtandaoni, ikiwa ni pamoja na Myanmar Now, mashambulizi yaliyolenga vituo vya kupigia kura na majengo ya serikali yaliripotiwa jana Jumapili katika angalau vitongoji vinne kati ya 100 vilivyokuwa vikiendesha vituo vya kupigia kura, huku maafisa wawili wa utawala wakiuawa.