Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anarerejesha mkono wa upendo usio wa kawaida kwa ishara maalum na ya nadra sana ya shukrani, akimpokea kansela Merz huko Ahmedabad katika eneo lake la nyumbani Gujarat, ambapo anapanga kumuonyesha eneo la kazi la shujaa wa kitaifa Mahatma Gandhi na pia tamasha la kitamaduni kwenye mto Sabarmati.
Mazungumzo ya kawaida ya kisiasa pia yanatarajiwa kufanyika katika mji wa nyumbani wa Modi.
Siku ya Jumanne safari inaendelea hadi Bengaluru, ambayo hapo awali ilikuwa Bangalore, kitovu cha tasnia ya teknolojia ya hali ya juu ya India, ambapo lengo linatarajiwa kuwa ushirikiano wa kiuchumi.
Kwa mara ya kwanza, Merz amepangwa kuambatana na ujumbe mkubwa wa biashara unaojumuisha zaidi ya watendaji 23 kutoka kampuni kubwa na za kati za Ujerumani, ikiwa ni pamoja na Siemens, Airbus Defense and Space na Thyssenkrupp Marine Systems.
Merz hajapangiwa kutembelea New Delhi, mji mkuu wa India, jambo ambalo si la kawaida kwa ziara ya kwanza ya uzinduzi.
Merz atanua sera za kigeni
Tangu aingie madarakani mwezi Mei, kansela Merz amewatembelea zaidi viongozi washirika barani Ulaya na Amerika Kaskazini. Sasa anakusudia kutoa kipaumbele zaidi kwa maeneo mengine ya dunia.
Mnamo Novemba alikuwa katika mikutano ya kundi la nchi 20 zilizostawi kiuchumi na zinazoinukia kwa kasi kiuchumi duniani na mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na bara la Afrika iliyofanyika nchini Afrika Kusini na Angola, na kabla ya hapo katika mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi nchini Brazil. Sasa Merz anaelekeza umakini wake moja kwa moja kwa bara la Asia.
Ni muhimu kukumbuka kwamba Merz anaitembelea India kabla ya China, soko muhimu zaidi la mauzo kwa biashara za Ujerumani barani Asia, na mbele ya Japan, mshirika pekee wa Asia katika kundi la nchi saba tajiri kiviwanda la G7, nchi za kidemokrasia zinazoongoza kiuchumi.
Ushirikiano mpya katika mpangilio mpya wa dunia
Umauzi wa Merz kuifanya India kuwa nchi ya ziara yake ya kwanza barani Asia unahusiana zaidi na mabadiliko na misukosuko ya sasa katika mpangilio wa dunia. Kutegemewa kwa ushirikiano uliothibitishwa kama vile ushirikiano kati ya Ulaya na Amerika Kaskazini kunazidi kupungua.
Kwa hivyo, Ujerumani inajitahidi kutanua ushirikiano wake na kupunguza utegemezi kwa mataifa makubwa, hasa Marekani katika nyanja ya usalama na China katika ushirikiano wa kiuchumi.
Kwa kuichagua India kama kituo chake cha kwanza, Merz anataka kuonyesha malengo yake mapya ya sera. India inabaki kuunganishwa kwa karibu na Urusi. Yote haya yanatarajiwa kuwa kwenye ajenda wakati wa ziara ya Merz.
Ulinzi: India inataka nyambizi za Ujerumani
India pia ina uhusiano wa karibu na Urusi kwa sababu vikosi vyake vya kijeshi bado vina vifaa vingi kutoka Moscow. Ujerumani ingependa kusaidia kubadilisha hilo.
Kampuni ya Thyssenkrupp Marine Systems kwa sasa inajadili uuzaji wa nyambizi sita kwa jeshi la wanamaji la India. Pia kuna nia ya India kutaka kununua ndege ya uchukuzi chapa Airbus A400M.
Hakuna mikataba thabiti inayoweza kuhitimishwa na kusainiwa wakati wa ziara ya kansela wa Ujerumani nchini India, ingawa tamko la nia ya wizara hizo mbili za ulinzi kuimarisha ushirikiano kati ya makampuni ya ulinzi ya nchi zote mbili litasainiwa.