Hii ni baada ya wizara za ulinzi za Ujerumani na India kusaini azma ya pamoja wakati wa ziara ya Kansela Friedrich Merz katika jiji la Ahmedabad, nchini India siku ya Jumatatu.

Merz aliyekaribishwa na Waziri Mkuu Narendra Modi, ambapo walitembelea sehemu inayohusishwa na shujaa wa taifa hilo Mahatma Gandhi amesema:

“Mmeshuhudia, tumetia saini makubaliano ya kihistoria. Azma moja inaeleza ushirikiano wa karibu zaidi kati ya sekta zetu za ulinzi katika nyanja za maendeleo na uzalishaji, pamoja na kukuza ubunifu na kuimarisha minyororo ya usambazaji duniani.”

Hadi sasa, hakuna mikataba maalum iliyosainiwa, lakini India inapanga kujenga manowari sita kwa kushirikiana na kampuni ya Ujerumani Thyssenkrupp Marine Systems (TKMS) mjini Mumbai, mradi unaokadiriwa kugharimu euro bilioni 8, sawa na dola bilioni 9.34.

Mkataba wa mradi huo unatarajiwa kusainiwa hivi karibuni na unaweza kufungua njia ya ushirikiano zaidi.

Merz amesema pia wanapaswa kukamilisha mazungumzo ya makubaliano ya biashara huru kati ya India na Umoja wa Ulaya.

Rais wa Tume ya Ulaya anatarajiwa kusafiri kwenda India mwishoni mwa mwezi huu na atasaini makubaliano hayo mara yatakapokamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *