Katika kutekeleza majukumu waliyopewa na nchi wanachama wa WHO, Dkt Ali Ahmed Yahaya ambaye ni kiongozi wa timu ya kupambana na usugu wa viuaji vya sumu wa WHO kwa Kanda ya Afrika anasema. 

“Tumetengeneza kanuni, miongozo na viwango ili wataalamu wa afya waweze kuzitumia katika kuhakikisha dawa zinazofaa za kuua viuaji vya sumu zinatolewa kwa viwango sahihi iwapo watalazimika kutibu maambukizi.”

WHO pia imeelekeza nguvu katika kutoa mafunzo, 

“Na pia tunahakikisha tunawajengea uwezo kupitia mafunzo na hii ni kwa watoa huduma wote wa afya katika ngazi mbalimbali kwenye sekta ya afya ili waweze kutumia vyema na inavyostahili Viaji vya sumu.” 

Na vipi kuhusu elimu kwa jamii? Dkt Yahaya anasema 

“Kwa ushirikiano wa karibu na nchi wanachama tunahakikisha kuna kampeni za mara kwa mara za kutoa taarifa kuhusu Viuaji vya sumu ili wawe na uelewa , kubadili tabia na kujua athari za matumizi yasiyofaa ya Viuaji vya sumu ikiwemo Antibiotics.”

WHO pia imeeleza umuhimu wa kila nchi kuwa na takwimu za tatizo hilo kwani ndio zinasaidia katika kufanya maamuzi na bila uwepo wake itakuwa ngumu kufanya maamuzi na mipango sahihi. 

Tayari WHO imekwishaweka majukwaa ya kuweka taarifa za chagamoto ya AMR na wanazisihi nchi wanachama kutumia majukwaa hayo kufanya uchambuzi wa taarifa na kisha kufanya maamuzi ya kupambana na usugu wa Viua Vijasumu katika nchi zao. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *