Ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upo nchini Tanzania kwa lengo la kuwasaidia raia wake wanaopewa hifadhi katika Mji wa Kigoma baada ya kutoroka mapigano yanayoendelea mashariki ya Kongo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ziara ya ujumbe huo nchini Tanzania inafuatia ile waliyofanya nchini Burundi ambapo Kinshasa inaendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Wakogomani waliopewa hifadhi katika nchi jirani.

Kinshasa imeimarisha juhudi za kuwasaidia raia wake waliokimbia mapigano nchini mwao, hatua hii ikijiri wakati ambapo ripoti ya Umoja wa Mataifa ikionyesha kuwa Wakogomani wakimbizi wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu katika kambi haswa nchini Burundi.

Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, wengi wao wanaishi katika hali mbaya ambapo wanakosa chakula, kukabiliwa na magonjwa hya mlipuko na hata kushambuliwa katika kambi hizo ambapo vifo vimeripotiwa.

Wakati huu mapigano yakiripotiwa katika baadhi ya maeneo ya mashariki, Shirika la Umoja wa Mataifa lakuhudumia wakimbizi (UNHCR), limeonya kuwa kambi za wakimbizi haswa nchini Burundi zimejaa kupita kiasi.

Kulingana na UNHCR, tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka uliopita, zaidi ya watu Elfu 84 wameingia nchini Burundi wakitokea katika jimbo la Kivu Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *