Nchini Benin, matokeo ya chaguzi mbili zilizofanyika sku ya Jumapili, Januari 11, yanatarajiwa kutangazwa siku ya Alhamisi, kulingana na Mkuu wa Mahakama ya Katiba, Cossi Dorothé Sossa. Jukwaa la uchaguzi la mashirika ya kiraia, ambalo lilituma waangalizi 1,200 kwa chaguzi hizi mbili, limetoa mahitimisho yake siku ya Jumatatu, Januari 12, likibainisha tofauti kubwa katika idadi ya wapiga kura kote nchini.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum mjini Cotonou, Magali Lagrange

Bila kutoa maelezo zaidi kwa wakati huu, jukwaa la uchaguzi la mashirka ya kiraia linabainisha tofauti kubwa katika idadi ya wapiga kura katika maeneo mbalimbali, pamoja na tofauti kati ya chaguzi hizo mbili zinazoashiria upendeleo miongoni mwa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge.

Vyama vitano vilikuwa vikishindana katika uchaguzi wa wabunge: vitatu kutoka muungano wa rais na viwili kutoka upinzani, ikiwa ni pamoja na Les Démocrates. Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani hakikuweza kushiriki katika uchaguzi wa madiwani, ambapo ni vyama vitatu pekee vilivyokuwa vikishindana.

Taarifa hiyo pia inazungumzia muktadha wa uchaguzi, hasa mageuzi ya kisiasa, kitaasisi, na kiuchaguzi ya miaka ya hivi karibuni ambayo yamebadilisha kwa kiasi kikubwa mfumo wa chama na sheria za kuandaa na kushiriki katika uchaguzi, na kusababisha mvutano kati ya wadau wa kisiasa.

Hoja nyingine iliyoibuliwa inahusu ucheleweshaji ulioonekana katika kuanza kwa upigaji kura katika vituo vya kupigia kura katika baadhi ya maeneo, kama vile Littoral na Atlantique, ingawa kipindi cha saa kumi cha upigaji kura kiliheshimiwa katika 95% ya vituo vya kupigia kura vilivyozingatiwa.

Masirika ya kiraia yanataka mazingira ya amani yadumishwe katika kipindi cha baada ya uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *