Katika barua hiyo aliyoichapisha kwenye mitandao ya kijamii  13.09.2025 Trump ameeleza kuwa yuko tayari kuiwekea vikwazo Urusi kama mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo yatakubali pia kufanya hivyo. Wito huo umetolewa wakati Urusi ikiendeleza vita vyake dhidi ya Ukraine ambapo imesema imefanikiwa kukidhibiti Kijiji cha Novomykolaivka katika mkoa wa Dnipropetrovsk. 

Licha ya madai ya Urusi, chanzo kutoka jeshi la Ukraine kimedai bado kijiji hicho kiko chini ya utawala wa Kyiv. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeeleza pia kuwa vikosi vyake vimezidungua droni 340 vya Ukraine katika siku moja iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *