
Mashambulizi ya anga ya Urusi yaua watu wasiopungua wanne usiku wa kuamkia leo Jumanne na kuwajeruhi wengine sita kaskazini mashariki mwa Ukraine, karibu na Kharkiv, gavana wa mkoa ametangaza leo Jumanne asubuhi, Januari 13.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la adui nje kidogo ya Kharkiv sasa imeongezeka hadi wanne. Watu sita pia walmejeruhiwa,” Oleg Synegubov ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram.
Mapema usiku huo, aliwaonya raia kuhusu “tishio la ndege zisizo na rubani za adui” na kutangaza vifo vya watu wawili.
Vikosi vya Urusi vilishambulia jengo linalomilikiwa na kampuni ya posta ya Nova Poshta, kulingana na ujumbe kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa mkoa wa Kharkiv ulioambatana na video.
Katika picha hiyo, wafanyakazi wa idara ya uokoaji wanaonekana wakipekua kifusi cha jengo kinachoendelea kutoa moshi na kumhamisha mtu kwenye machela usiku, shirika la habari la AFP limeripoti.