#HABARI: Wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa elimu ya juu nchini ikiwa ni pamoja na utoaji wa fursa za masomo kwenye mataifa tofauti ulimwenguni, wadau wa maeendeleo katika Sekta ya elimu wamesema wataendelea kuunga mkono juhudi hizo ili ziweze kuzalisha wasomi kwenye nyanja mbalimbali ya elimu ya juu.
Kadiri miaka inavyokwenda mbele Sekta ya elimu nchini Tanzania imetajwa kuimarika ikilinganishwa na hapo awali kutokana na uwekezaji ambao umefanywa na Mamlaka husika jambo ambalo limeendelea kuzalisha wataalamu wanaotumika kwenye uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Ingawa kumekuwepo na mafanikio hayo lakini inaelezwa kuwa ipo sehemu kubwa ya wanafunzi ambao wana uhitaji wa kwenda kupata masomo ya elimu ya juu kwenye mataifa tofauti ulimwenguni.
Ili kurahisisha hilo Shirika lisilo la kiserikali la Akili Education linaamua kuunganishani nguvu ya pamoja na Chuo Kikuu cha KHALSA kilichopo nchini India kwa lengo la kutoa fursa za masomo kwa wanafunzi wa ndani ya nchi kwenda kusoma India.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: Tuma 1,000/- kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M-Pesa, au Halopesa kwenda namba ya kampuni 222223. Kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates