Wanamgambo hao wa Arakan kupitia chaneli yao ya telegram leo Jumamosi wamebainisha kwamba mashambulizi yalizilenga shule mbili binafsi za sekondari. Wanafunzi waliouawa wana umri kati ya miaka 15 na 21 wakati wanafunzi wengine 22 wamejeruhiwa. Jeshi la Myanmar hajatoa kauli yoyote kuhusu mashambulizi ya leo.

Mzozo wa Rakhine ni sehemu ya machafuko yaliyojaa umwagaji damu yanayoitesa Myanmar, tangu jeshi lililpoipindua serikali ya kiraia ya  Aung San Suu Kyi mwaka 2021. Tangu hapo, watawala wa kijeshi wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa makundi yanayowapinga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *