
Miaka saba ya kiangazi nchini Morocco imefikia kikomo baada ya mvua za msimu wa baridi kali, Waziri wa Maji Nizar Baraka amesema siku ya Jumatatu.
Mvua za msimu huu wa baridi ni 95% zaidi ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka mmoja uliopita na 17% zaidi ya wastani kwa msimu, Baraka amewaambia wabunge.
Kujaza mabwawa kumeongezeka kwa 46%, huku hifadhi za maji zikijaa pomoni, takwimu rasmi zinaonesha.
Mvua hizo zimeleta afuweni kubwa kwa sekta ya kilimo baada ya miaka kadhaa ya uhabad wa maji.