Wagombea Urais Uganda 2026Wagombea Urais Uganda 2026

Uganda itakuwa na Uchaguzi Mkuu Januari 15, 2026.Kuna jumla ya wagombea 8 wanaowania nafasi ya urais wa nchi hiyo.

Rais Yoweri Museveni ambae amekuwa madarakani tangu 1986 ni miongoni mwa wagombea wanaotaka kuchaguliwa kwa awamu nyengine.

Ahadi yake kwa wananchi Uganda ni kuifanya nchi hiyo kuwa ya kipato cha kati kwa kukuza viwanda, kuongeza thamani ya mauzo ya nje ya kilimo kama vile kahawa na pamba na kufaidika na kuanza kwa uzalishaji wa mafuta unaotarajiwa baadaye mwaka huu.

Msanii maarufu Robert Kyagulanyi mwenye umri wa miaka 43 anaonekana kuwa mpinzani mkuu wa Museveni akipeperusha bendera ya chama cha Nataional Unity platform(NUP).

Akifahamika kwa jina la ‘Bobi Wine’ na pia “rais wa gheto” wakati mmoja, anaonekana kujumuisha matarajio ya vijana ya mabadiliko na pia ameapa kukomesha ufisadi, kuimarisha ajira kwa vijana na kupitia upya mikataba na makampuni ya kimataifa ya mafuta ikiwa hayapendelei maslahi ya Waganda.

Hili ni jaribio lake la pili katika nafasi ya juu baada ya kushiriki katika kura za 2021.
Robert Kasibante mwenye umri wa miaka 38 mgombea chini ya Chama cha National Peasants Party( NPP) alijulikana kwa muda mrefu kwa kuendesha shule ya urembo huko jijini Kampala.

Sasa ndiye mgombea wa chama hicho kilichoanzishwa mwaka 2004. Mpango wake ni kukuza sekta ya kilimo ambayo inategemewa zaidi na wakulima wadogo ili kuwawezesha kupata manufaa zaidi.

Frank Bulira Kabinga ndiye mgombea urais wa Chama cha Revolutionary People’s Party (RPP) katika uchaguzi mkuu wa 2026.

Alikuwa mwalimu wa shule ya upili, Bulira ni mtetezi mkubwa wa siasa za ushirikisho na mageuzi mengine ya utawala.Joseph Mabirizi ana taaluma ya Uinjilisti na anajulikana kwa kuanzisha makanisa katika sehemu za nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *