Mwaka mpya 2026 wakazi wa Gaza wana matarajio makubwaMwaka mpya 2026 wakazi wa Gaza wana matarajio makubwa

Wananchi hao wanasalia kuwa na sintofahamu kubwa kuhusu mustakabali wa maisha yao baada ya miezi kadhaa ya vita na uharibifu. Hata hivyo kama msemo wa kiswahili usemao “Hakuna marefu yasiyo nan cha” wananchi hawa sasa wanamatumaini baada ya sitisho la mapigano lililopitishwa mwaka 2025.

Sasa mwaka mpya wa 2026 ukianza wananchi bado wanakabiliwa na changamoto za ugumu wa maisha baada ya vita lakini mwanga wa matumaini unaonekana. Sauti sasa ni za watoto wakicheza badala ya makombora kama ilivyokuwa wakati wa vita.

Makrama Ahmad, Raia Mpalestina ambaye ni mwenyeji wa Gaza.

United Nations

Makrama Ahmad, Raia Mpalestina ambaye ni mwenyeji wa Gaza.

Wapalestina waliokimbia makazi yao au wengine makazi yao kuharibiwa wakati wa vita kwasasa wanaishi katika makazi ya muda ya wakimbizi wa ndani na wanaelezea kuwa na matumaini kwamba mwaka mpya unaashiria mabadiliko makubwa katika maisha yao. 

Ni mabadiliko gani hayo wanayotarajia kwa mwaka huu? Makrama Ahmad anasema “Tunatumaini Mungu atatulipa fidia kwa ajili ya nyumba zetu zilizoharibiwa. Tulipoteza watoto wetu, wengine walijeruhiwa, na tunamshukuru Mungu.”

Naye Akram Abu Sal’a anaongeza kuwa “Tunatumaini kwamba mwaka 2026 utakuwa bora kuliko mwaka 2025, na kwamba vita na mateso vitaisha.” 

Kama inavyofahamika katika vita wanaoteseka zaidi ni wanawake na watoto. Akiwa amempakata mjukuu wake, ameketi nje ya hema lake la msaada kutoka Umoja wa Mataifa Na‘ma Al-Khawaja anasema “Mwaka 2026, natumaini kupata matibabu, nifanyiwe upasuji na kuona siku njema zaidi zijazo”. 

UN News

Na‘ma Al-Khawaja, mwanamke mzee wa Kipalestina, akiwa amembeba mjukuu wake mbele ya hema lao kaskazini mwa Jiji la Gaza.

Wafaa Al-Khawaja, ni mkazi wa Gaza na anasema “Natamani tungeweza kuisha kama watu wengine duniani kote wanavyoishi. Leo, watoto wetu hawana fursa ya kupata elimu wala kitu chochote kile.”

Bi. Kamal Abu Hsheish akiwa amesimama nje ya hema lake huko mjini Gaza anasema “Natumaini tutarejea katika maisha yetu kabla ya vita na tutakuwa na hali nzuri. Mungu akipenda.”

Bi Noha Abu Amsha ana matumaini ya furaha “Tunatumaini kwamba mwaka 2026 utakuwa mwaka uliojaa furaha na fanaka, kwamba wanajeshi wataondoka kabisa katika Ukanda wa Gaza, na kwamba watu watarudi katika makazi yao. Hata kama tukirudi kambini, tutaishi kwa usalama na utulivu.”

Naye Shifaa Abu Halima anasema “Inatosha kwamba tunaishi kwenye mahema na yanazama kwa sababu ya mvua, na hakuna mtu anayetuhurumia. Hatuna chochote, hata nguo hazipatikani.” 

A young Palestinian girl wearing a Santa Claus outfit, standing in front of tents of displaced families in northern Gaza City.

Msichana mdogo wa Kipalestina aliyevalia vazi la Santa Claus, akiwa amesimama mbele ya mahema ya familia zilizopoteza makazi yao kaskazini mwa Jiji la Gaza.

Ama hakika inatosha, madhila yametosha na juhudi za kidiplomasia zinaendelea kuhakikisha Gaza kuna amani ya kudumu. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *