Real Madrid yaachana na Xabi AlonsoReal Madrid yaachana na Xabi Alonso

Kulingana na Madrid, Alonso ameondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili lakini hatua hiyo ilifuatia kipindi kigumu kilichodumu kwa karibu miezi minane na ilikuja siku moja baada ya Madrid kufungwa 3-2 na Barcelona katika fainali ya Kombe la Super Cup la Uhispania iliyochezwa Saudi Arabia.

Nafasi ya Alonso ilijazwa muda mfupi tu baada ya kutangaza kuondoka na kocha wa zamani wa vijana Arbeloa, ambaye alicheza pamoja na Alonso wakiwa Madrid, Liverpool na timu ya taifa ya Uhispania, na kushinda Kombe la Dunia mwaka 2010.

“Real Madrid inapenda kutangaza kwamba, kufuatia makubaliano ya pande mbili kati ya klabu na Xabi Alonso imeamriwa kuhitimisha kipindi chake kama kocha,” ilisema taarifa. “Real Madrid itakuwa ni nyumbani kwake siku zote.” Klabu hiyo pia iliishukuru timu iliyofanya kazi pamoja na Alonso.

Kombe la Super Cup la Uhispania 2026 | Fainali | FC Barcelona dhidi ya Real Madrid | Fermin Lopez akipambana na Eduardo Camavinga
Kombe la Super la Uhispania – Fainali – FC Barcelona dhidi ya Real Madrid – Uwanja wa King Abdullah Sports City, Jeddah, Saudi Arabia – Januari 11, 2026 Fermin Lopez wa FC Barcelona akicheza na Eduardo Camavinga wa Real MadridPicha: Vincent West/REUTERS

Alonso alijiunga na timu hiyo huku kukiwa na matarajio makubwa, akichukua nafasi ya Carlo Ancelotti katikati ya shinikizo kubwa. Hata hivyo katika kipindi chake amejikuta katika sintofahamu kutokana na mivutano na baadhi ya wachezaji ikiwa ni pamoja na Vinicious Junior na ripoti zilizosambaa mitandaoni zilizosema ameshindwa kuwadhibiti wachezaji wake.

Amefanikiwa kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi 34, katika michuano mbalimbali, na akishinda 24, droo 4 na alishindwa mechi 6. Madrid ilishinda El-Clasico ya kwanza ya msimu huu mwezi Oktoba kwa 2-1, lakini bado iko nyuma ya Barcelona kwa pointi 4. Jumatano itakutana na Albacete katika raundi ya 16 ya Kombe la Copa del Rey.

Akiwa mchezaji, Arbeloa aliisaidia Madrid kushinda mataji manane kuanzia 2009-16, yakiwemo makombe mawili ya Ulaya na moja la ligi ya Uhispania. Arbeloa pia aliisaidia Uhispania kushinda Kombe la Dunia la 2010 na Mashindano ya Ulaya ya 2008 na 2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *