Haiti: Vocha za chakula zinarejesha heshima na uhuru kwa familiaHaiti: Vocha za chakula zinarejesha heshima na uhuru kwa familia

Akiwa amesimama nje ya jengo lililopakwa rangi ang’avu kusini-mashariki mwa Haiti, kwenye lango la duka lenye shughuli nyingi linaloitwa Gods Will Depot, ambako magunia ya chakula yamepangwa hadi darini, Ketia anaangalia rundo la bidhaa alizochagua kwa ajili ya familia yake: gunia kubwa la unga, pakiti za tambi (spaghetti), maziwa ya boksi na sabuni kadhaa.

Mwanamke mmoja nchini Haiti, anayejulikana kama Ketia, ameonekana akibeba sanduku la misaada iliyopokelewa kupitia mfumo wa voucher wa Programu ya Chakula Duniani, ambayo husaidia familia kununua bidhaa kutoka kwa wauzaji wa ndani baada ya dhoruba.

© WFP/Sylvain Barral

Ketia anapokea msaada wa chakula uliolipwa kwa kutumia vouchers.

Ketia na mume wake wote ni walimu. Kabla ya Kimbunga Melissa kupita katika eneo la Karibiani mwezi Oktoba uliopita, waliweza kuwahudumia watoto wao watatu. Hata hivyo, dhoruba ilipopiga, jamii yao ya pwani ya Petit Goâve ilikuwa miongoni mwa zilizoathirika zaidi.

Nilipoteza kila kitu nilichokuwa nacho: samani, gari langu, kila kitu kilichokuwa nyumbani,” amelalamika Ketia.

Ketia na familia yake ni miongoni mwa takribani watu 225,000 wanaopokea msaada kutoka WFP baada ya dhoruba hiyo. Anapokea msaada kupitia mfumo wa vocha unaowezesha familia kununua bidhaa kutoka kwa wauzaji walioteuliwa, mpango unaosaidia walioathirika huku pia ukichochea uchumi wa ndani.

Duka linatumia mfumo wa kielektroniki unaorekodi miamala inayoendelea, na WFP humlipa muuzaji. Ni njia nzuri ya kusaidia familia zilizoathirika, kwa sababu badala ya kwenda kupokea msaada kwenye mgawo, mnufaika anakuwa kama mnunuzi wa kawaida, akiingia sokoni.” ameeleza Channon Hachandi, mkuu wa mnyororo wa ugavi wa WFP Haiti

Hata kabla ya Kimbunga Melissa, zaidi ya nusu ya wakazi katika maeneo yaliyoathirika zaidi tayari walikuwa wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula, ishara ya mgogoro mkubwa wa kibinadamu ambao Haiti imekuwa ikikabiliana nao kwa miaka mingi.

Channon Hachandi, ameendelea kusisitiza kuwa  hii ni njia nzuri ya kusaidia familia zilizoathirika badala ya kupokea msaada kwenye mgawo, wanakuwa kama wanunuzi wa kawaida sokoni.

Dhoruba hiyo ilisababisha vifo vya zaidi ya waHaiti 40, na wengine wengi walipoteza nyumba, biashara na mali zao. Katika eneo linalotegemea sana kilimo cha kiwango kidogo, mashamba yaliharibiwa kwa kiasi kikubwa na mavuno yakapotea karibu yote.

WFP ilitoa msaada kabla, wakati na baada ya kimbunga. Kwa kushirikiana na serikali, shirika hilo lilituma ujumbe wa maandishi wa tahadhari ya mapema milioni 3.5 kupitia simu za mkononi, na kutoa malipo ya fedha taslimu ili kuwasaidia watu kujiandaa na kupunguza athari za kimbunga.
Wakati wa dhoruba yenyewe, familia zilizohamia kwenye makazi ya muda zilipatiwa mgao wa chakula. Mara baada ya hapo, wakati familia zilipotathmini uharibifu, mgao wa chakula wa siku 15 ulisambazwa.

Maoni ya hewa ya jumuiya ya Haiti iliyoathiriwa na dhoruba, ikionyesha nyumba, barabara, na magari, na WFP ikitoa msaada wa chakula kupitia mfumo wa voucher.

© WFP/Sylvain Barral

Kampuni ndogo ya Petit Goâve kusini mashariki mwa Haiti inarudi nyuma baada ya Kimbunga Melissa mnamo Oktoba 2025.

Ili kusaidia jamii kurejea katika hali ya kawaida, mwitikio umebadilika na sasa unajumuisha utoaji wa fedha taslimu na vocha, hivyo kuwapa familia kile ambacho WFP inakiita “heshima ya kuchagua.”
Kwa sasa, takribani asilimia 10 ya wahaiti wanaopokea msaada baada ya Kimbunga Melissa, wananufaika na mpango wa vocha njia ambayo WFP inalenga kuipanua.

Wilfred Nkwambi, Mkuu wa Programu za WFP nchini Haiti, amesisitiza kuwa vocha ni zaidi ya njia ya kuwalisha watu, ni msukumo mpya kwa uchumi wa ndani.
Katika duka hili pekee, mmiliki ameajiri watu wanane wa ziada kwa ajili ya usambazaji huu wa chakula. Katika eneo hili la Petit Goâve, kuna maduka mengine matano, yanayoajiri jumla ya watu 40, wengi wao wakiwa wanawake na vijana. Sio tu kwamba ni jambo jema kwa wanufaika, bali pia kwa wafanyabiashara wa mji na wazalishaji wa ndani,” ameeleza Bw. Nkwambi.

Wakati huohuo, WFP huajiri vibarua wa siku kwa ajili ya shughuli za ugavi na usafirishaji, hivyo kuzalisha kipato cha ziada kwa familia za eneo hilo. Mbinu hii inanufaisha kila mtu, ikibadili msaada wa kibinadamu kuwa chachu ya uokoaji wa kiuchumi.

Kwa mujibu wa WFP, kuweka heshima na uhuru wa kuchagua kuwa kiini cha uingiliaji kati kunaonesha kuwa msaada wa kibinadamu unaweza kwenda sambamba na uhimilivu wa watu wa Haiti.
Ketia ameshukuru WFP kwa usambazaji wa vocha za chakula, akisema kuwa hawatakosa chakula katika wiki zijazo, na wana nafasi ya kuanza kujenga upya maisha yao, amesema hivi alipokuwa akipakia bidhaa zake kwenye pikipiki ya usafiri na kurejea kwa familia yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *