MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, amesema Zanzibar ina mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na utamaduni kutokana na historia yake ya mwingiliano wa tamaduni kupitia biashara ya monsuni.

Amesema Mji Mkongwe wa Zanzibar, ulioorodheshwa na UNESCO, unaendelea kuwa “Urithi Hai” unaoishi katika maisha ya wananchi. Mama Mariam Mwinyi aliyasema hayo mjini Sharjah(UAE) katika Tamasha la Fasihi na Kazi za Sanaa za Afrika (SFAL).

Mama Mariam Mwinyi ametoa pongezi kubwa kwa “Sharjah Book Authority” kwa kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni kati ya Afrika na Ulimwengu wa Kiarabu. Aidha amesema dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kulinda na kuendeleza urithi na utamaduni kama msingi wa utambulisho wa taifa na maendeleo endelevu.

Kupitia ZMBF, alitaja kilimo cha mwani kama mfano wa urithi unaowanufaisha zaidi ya wanawake na vijana 1,200 wa Unguja na Pemba. Katika tamasha hilo, Zanzibar iliwakilishwa na wasanii na wabunifu waliowasilisha kazi za sanaa, uchongaji wa milango ya Kizanzibari, usimulizi wa hadithi, uandishi wa vitabu na mavazi ya kitamaduni. SOMA: ‘Hapana tena ukatili wa kijinsia’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *