#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt

#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Rais Samia amechapisha taarifa hii na kueleza kuwa anawatakia kila la kheri katika maandalizi ya safari yao ya kwenda kuomba ridhaa ya wananchi kupitia Sanduku la kura, kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025.

Rais Samia ameandika ‘Ninawapongeza wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Ninawatakia kila la kheri katika maandalizi ya safari yenu ya kwenda kuomba ridhaa ya wananchi kupitia sanduku la kura, kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025.

Mwenyezi Mungu awatangulie, awaongoze na kuwafanikisha.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *