Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani, limewataka madereva waliokosa sifa za kupata leseni kurudia mitihani ya udereva inayotolewa na jeshi hilo ili waweze kukidhi vigezo vya kisheria na kupata leseni halali.
Kauli hiyo imetolewa na Mussa Manyama, Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, wakati akijibu malalamiko ya madereva yaliyowasilishwa kwa kikosi hicho.
Amesisitiza kuwa lengo la hatua hiyo ni kuimarisha usalama barabarani, kupunguza ajali, na kuhakikisha kuwa madereva wote wanaendesha vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates