Naibu waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amechukizwa na wakandarasi wanaojenga Mradi wa Maji wa Miji Ishirini na Nane unaotekelezwa katika kata ya nyabiyonza wilayani Karagwe Mkoani Kagera ambao unghalimu zaidi ya shilingi Bilion 64 za Kitanzania ambao umeshindwa kukamilika kama ilivyopangwa kwenye Mkataba wao wa Awali.