Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uwenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Labani Kihongosi, leo tarehe 17, jamuari 2026 ametangaza kuanza kwa ziara ya kichama ya kitaifa itakayohusisha mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Jakaya Convention Centre jijini Dodoma, Ndugu Kihongosi amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kuendelea kushirikiana na wananchi na wanachama wa CCM katika kulinda amani, umoja na maendeleo ya Taifa, sambamba na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi moja kwa moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *