#HABARI: Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Stephano Loto, amefariki dunia baada ya kushambaliwa vibaya na kundi la fisi waliomjeruhi sehemu mbalimbali na kupelekea umauti, tukio lililotokea katika Kijiji cha Dohomu wilayani Babati mkoani Manyara.

Loto mwenye umri wa miaka 60 alishambuliwa usiku wa kuamkia leo alipokua akitoka shambani kulima

Baada ya kushambuliwa, mwili wa marehemu uligawanywa vipande vipande na mnyama huyo, Mashuhuda wanasema baadhi ya viungo vya mwili wake vilikutwa vimetawanyika shambani, jambo lililoacha simanzi, hofu na mshtuko mkubwa kwa wananchi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiomba Serikali pamoja na mamlaka husika, ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) na Idara ya Wanyamapori, kuchukua hatua za haraka kudhibiti wanyama hao wakali, wakisema wamekuwa tishio kubwa kwa usalama wao na uchumi wa familia zao.

Jeshi la Polisi mkoani Manyara tayari limeuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya taratibu za uchunguzi na mazishi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *