Mjasiriamali Dorice Mushi, ambaye amepitia hali ngumu ya maisha kabla ya kufanikiwa kimaisha, amesema kuwa mafanikio yoyote huanza na Mungu katika kila jambo. Ameeleza kuwa ili kufanikiwa katika malengo anayoyaweka, ni muhimu mtu ajue anachokitaka katika maisha, awe na malengo yaliyo wazi na ajitume kwa bidii, kwani jitihada ni njia bora ya kutimiza malengo.
Aidha, Dorice ameeleza namna alivyopambana akiwa na umri mdogo wa miaka 23 na kufanikiwa kujenga nyumba ya wazazi wake kijijini alikozaliwa. Ameongeza kuwa akiba ilikuwa nguzo muhimu katika safari yake ya mafanikio, akiamua kuacha vitu vingi ili kutimiza lengo lake kuu la kuwajengea familia yake nyumba ya kisasa.
✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTVUpdates