#HABARI: Mvua kubwa na upepo mkali mkoani Ruvuma, umebomoa bweni la dharura katika Shule ya Sekondari Mateteleka, Halmashauri ya Madaba.

Jengo hilo, ambalo awali lilijengwa na wananchi kama bwalo la chakula, lilikuwa likitumiwa na wanafunzi wa kiume kama sehemu ya kulala kutokana na uhaba wa miundombinu shuleni hapo.

Kufuatia maafa hayo, Mbunge wa Madaba, Mhe. Omary Msigwa, ametoa msaada wa bati 90 ili kusaidia ukarabati wa jengo hilo. Mkuu wa shule hiyo, Bw. Godfrey Njovu, ameshukuru kwa msaada huo huku akieleza umuhimu wa kurejesha bweni hilo haraka kwa ajili ya usalama na ustawi wa wanafunzi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *