Ndani ya hifadhi ya msitu wa asili wa Uzungwa Scarp inayopatikana mpakani mwa mikoa ya Iringa na Morogoro, kumeibuliwa kivutio kipya cha utalii. Ni maporomoko marefu ya maji yanayojulikana kwa jina la Funo.
Eneo hilo, ambalo liko chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), limekuwa gumzo si kwa makeke, bali kwa kelele za anguko la maji linalovutia. Mwenzetu Muhammad Nyaulingo ametembelea maporomoko hayo na kuandaa taarifa hii.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi